TBS na TRA kikaangoni upotevu wa makontena 100 bandarini

Serikali imewataka baadhi ya wafanyakazi wa shirika la viwango Tanzania (TBS), walioshirikiana na wenzao wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), kupitisha makontena zaidi ya 100 bila kukaguliwa na shirika hilo katika bandari ya Dar es Salaam kujisalimisha.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alitoa agizo hilo Jumapili hii wakati akizindua baraza la wafanyakazi wa TBS.
“Nimeanza kukusanya orodha ya majina ya watu waliosaidia kupitisha makontena haya na nikija nayo hawatapona,” alisema Mwijage. Aliwataka wote wanaojijua kuhusika kujisalimisha mapema na kutubu ili wasamehewe kabla ya hatua kali kuchukuliwa.
Makontena hayo yalipitishwa katika bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni bila ya kuthibitishwa na TBS.                                                                                                                                                             BY MP DULLY NEWZ

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.